KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
SEHAMU YA TANO
Jijini Mwanza huu ni moja ya mikoa ipatikanayo inchini Tanzania pia mkoa huu unasifika kwa kuwa na watu wakarimu sana kwani umekusanya makabila mengi sana yakiwemo ya wasukuma ,wahaya.na mengineyo.
Ilikuwa imepita wiki moja tangu tukio la mauaji ya kinyama kutokea jijini Dar kwa kuuwawa kwa msichana na muuwaji asijulikane hali bado ilikuwa katika sintofahamu maana ilikuwa ngumu kutambua chanzo cha mauaji hayo wengine walikuwa wakisema kuwa viongozi walikuwa wanatoa kafara maana ulikuwa umebaki mwaka mmoja uchaguzi mkuu ufanyike nchini Tanzania kila mtu alikuwa akisema kwa namna alivyo kuwa akijua yeye mwenyewe ..
Kelele za furaha na shangwe zilikuwa zikisikika kutoka katika basi moja ambalo huwa linafanya kazi ya usafirishaji kutoka mwanza to mbeya lakini kwa siku hii lilikuwa limebeba wanafunzi ambao walikuwa wamelikodi kwa ajili ya kuwasafirisha kwenda mkoa wa jirani kutoka Jijini Mwanza ..lakini ndani ya basi hilo kulikuwa na mtu ambaye wakati wote alikuwa kimya tuu ambaye naye alikuwa amevalia uniform za shule hiyo yeye alikaa nyuma kabisa huku akionekana kuwa ni mwenye mawazo mengi sana ..Wanafunzi wale waliendelea kupiga kelele ambazo zilikuwa zikimkela dereva wa basi hilo pamoja na kondakta wake wote walikuwa wamechukia na kutamani wanafunzi wale wa kike kunyamaza lakini ilikuwa ngumu sana kuwatuliza baada ya mda mrefu atimaye usiku ulianza kuingia na mmoja baada ya mmoja alianza kunyamaza hali hadi ikafikia gari zima wakanyamaza na pakawa kimya huku wakionekana kuwa wamepitiwa na usingizi kasoro mwanafunzi mmoja yule ambaye aliyeonekana kuwa na mawazo mengi yeye alikuwa anatembea kuelekea kwa dereva na kumuomba kushuka akajisaidie haja kubwa maana alidai kuwa tumbo lilikuwa likimsumbua ,dereva hakujali kwa kuwa alikuwa ni mmoja wa wanafuzni katika gari hilo ..fanya fasta dogo alisema dereva huku akipata nafasi ya kuwatazama wanafunzi ambao walikuwa wamelala kama watu waliolewa "
"Oyaaa embu mcheki huyo dogo mbona kachelewa hivi anajiasidia kokoto nini"ilikuwa ni sauti ya dereva huku akitokwa na tusi kali lililokuwa nikimuhusu hasa konda wake ambaye alikuwa anasinzia "saa moja baadae"Broo mbona huyu dogo simuoni afu na hawa wengine wamelala staili gani hii kama wamelewa"Ilikuwa ni sauti ya konda huku akiwa tayari ndani ya basi akifanya zoezi la kuwashtua wanafunzi hao lakini kila aliye kuwa akimshtua alikuwa kimya tu
"Ramaaa wanafunzi wamekufa "aliongea konda huku akiwa katika mshangao
"Unasemaje "aliuliza dereva huku akija nyuma kwaajili ya kuwatazama
Mungu wangu !ulikuwa ni mshangao maana mda mfupi tu walikuwa wakiimba alafu sasa hivi wamekufa
Konda tayari alikuwa kashika simu yake na kupiga namba kisha kueleza tukio hilo la kuuwawa kwa wanafunzi bila kumuona muuwaji .......MUUAJI NDANI YA MWANZA USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA
Monday, 9 April 2018
New
About Hamadi abel
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment