- HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Monday, 9 April 2018

KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769


                                                               SEHEMU YA SITA
Jijini Dar zilikuwa ni taarifa za majonzi ambazo zilikuwa tayari zimeshaenea karibu inchi nzima huku vyombo vya habari vikionekana kufanya kazi yake ipasavyo kwa kuweza kusambaza habari ya wanafunzi walipkufa ndani ya gari na muuaji kutimkia porini huku polisi wakiendela na uchunguzi wa suala hilo..Makao makuu ya polisi ..ilikuwa majira ya saa saba mchana ambapo kiliitishwa kikao cha gafla na I.G.P kwaajili ya kujadili hali ya usalama kwa ujumla pamoja na matukio ya uuaji kuzidi kushika kasi hapa inchini..
"Ndugu zangu nafikiri nyie wenyewe mmekuwa  mnajionea hali ilivyo kwa sasa inchini"ilikuwa ni sauti ya I,G,P kwenda kwa makamishna wa polisi na viongozi wengine wa usalama kutoka kila mkoa wa Tanzania hivyo naomba  Tanzania ibaki kuwa nchi ya amani maana muuwaji hawezi kuwa anauwa kila mkoa na sisi jeshi la polisi tuko kimya bila kuchukua hatua yoyote huu ni udhaifu tunataka kuuonyesha mmnaona kama wanafunzi hao wamekufa bila hatia na ni pengo kubwa kwa taifa maana tumepoteza ndugu zetu wengi..
Siku iliyo fuata Rais alitangaza kuwa bendela ya Taifa ifungwe nusu mlingoni ikiwa ni ishara ya kuwaenzi wanafunzi hao na pia kukemea matukio ya kigaidi ambayo sasa yanazidi kushika kasi inchini na kusema kuwa jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa namba moja ambaye kwa namna moja ama nyingine atakuwa akijua chanzo cha mauaji haya hivyo ningependa  mzidi kuonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kutokomeza janga hili ambalo linataka kuikumba Tanzania hayo yalikuwa ni maneno kutoka kwa Rais wa jamuhuri ya Tanzania...
"Hapana mimi siusiki kwa kitu chochote"ilikuwa ni sauti kutoka katika chumba cha upelelezi ambacho bwana John alikuwa akihojiwa tangu siku ile tukio lilipotokea mpaka sasa bado yeye alituhumiwa kuwa ndio muhusika namba moja katika matukio au huenda atakuwa anawajua wahisika na kutakiwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kutokomeza janga hili..
Wakati yote haya yakiendelea kutokea nchini Tanzania..ndani ya gereza la segerea kulikuwa kuna mtu ambaye yeye tangu afikishwe pale inasemekana hajawahi kutamka neno lolote na alionekana kama kichaaa kwani mda wote yeye aliutumia kutazama juu tu hadi pale alipokuwa akipata kipigo kikali kutika kwa askari magereza inasemekana yeye alihukumiwa kwa kosa la kumuuwa  mwenzake kwa kumchoma kisu wakati wakiwa katika moja ya kumbi za starehe jijini Dar ...ndiko ambako John alikotupwa katika gereza hilo....JOHN GEREZANI JE MUUWAJI NI NANI USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA

No comments:

Post a Comment