KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
SEHEMU YA SABA
Ilipoishia bado tukiwa bado tuko ndani ya gereza ambako tunatambua kuwa John ndiko alikokuwa amefungwa kwa kosa la mauaji huku akiwa anasubiri siku ya kusikilzwa kwa kesi yake......Songa nayo "dogo ilisikika sauti kutoka katika kona moja ndani ya gereza hilo kutokana na kuwa giza nene hivyo ilikuwa ngumu kufahamu aliyekuwa akiiitwa ni nani."dogo sauti ile iliendelea kuita hadi pale niliposikia kuwa niliekuwa nikiiitwa nilikuwa ni mimi maada mda wote nilikuwa nimejiinamia huku nikiwa nalia"Nikajikuta namsogelea mtu yule ambaye alikuwa akisemekana kuwa ni kichaa maana hakuwahi kuongea tangu afikishwe ndani ya gereza hilo ilikuwa ni kama maajabu kwa mtu yule kuweza kuongea tena akinisemesha mimi ambaye ni mgeni.
Mbona mda wote unalia "aliuliza yule bwana
"Hapana mbona nipo kawaida nilijibu huku nikiwa na mashaka na mtu huyo"
"Najua unaweza ukawa umesingiziwa hadi kuwa hapa"alisema bwana yule huku akiwa ananitazama kwa macho makali ambayo yalinifanya niamini kuwa alikuwa ni kichaa
"Ni story ndefu sana "nilijikuta nikiwa nimeeanza kumzoea bwana yule kutokana na jinsi alivyokuwa akizungumza na mimi ilikuwa ni kama mtu anaye fahamu juu ya tatizo la mauaji ama na yeye yamemkuta kama yaliyo nikuta mimi"
"Makao makuu"ulikuwa ni mpango ambao ulikuwa unaandaliwa kwaajili ya kumtafuta muhusika wa mauaji yanayo endelea kutokea nchini Tanzania"Mpango ambao ulisemekana kuwa utahusisha wafungwa wawili ambao ilisemekana kuwa wawo ndio wanaweza kuwa njia ya kumfikia muuaji
Pia ulikuwa ukihusisha vijana mahili kutoka katika jeshi la polisi ..."Ulikuwa ni ujio wa kikosi maalumu kutoka katika jeshi la polisi sasa walikuwa wakielekea katika gereza kwaajili ya kuchukua wafungwa ambao wao walidai kuwa watakuwa msaada kulisaidia jeshi la polisi ...Alianza yule bwana kuitwa ambaye alisemekana kuwa ni kichaa lakini kwangu mimi niliona kuwa sio kichaa ..mala ikawa zamu yangu mimi kuitwa na kutoka kisha nikabidhiwa kila kitu changu na kutoka nje bila kujua kwanini nilikuwa hapo nje.....Ikatoka amri ya kupanda ndani ya gari ambalo kwa muonekano lilikuwa halipitishi risasi lakini sikufanikiwa kumuona yule bwana zaidi ya kuwaona maaskari wawili wakiwa na mitutu ya bunduki huku wakiwa makini zaidi ya nilivyokuwa ni kitegemea asalaleee kweli nilikuwa katika ulinzi mkali utazani gaidi ...
Ilikuwa ni masaa machache tangu nitoke katiaka gereza hilo sasa tulikuwa mezani pamoja na mkuu wa jeshi la polisi jambo ambalo mpaka sasa nilikuwa bado sijalielewa ..
"John kuanzia sasa utashilikiana na huyu bwana hapa katika kuusaka ukweli wa mauaji haya mtapata kila kitu ambacho mtakuwa mkiihitaji na pia bwana Omary kuanzi sasa utakuwa na huyu bwana "alikuwa akiambiwa yule bwana amabye alijulikana kwa jina la Omary ambaye sasa alikuwa kimya tu kana kwamba ni bubu"Alimaliza na kisha kutimka huku mimi pamoja na Omary tukiwa tumeachiwa kazi ngumu ya kumtafuta muuaji ili mimi niwe huru pamoja na familia yangu
HAYA SASA NDANI YA KIBALUA CHA KUMTAFUTA MUUAJI USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Friday, 13 April 2018
New
About Hamadi abel
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment