MPANGO WA KANDO - HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Monday, 19 March 2018

MPANGO WA KANDO

MPANGO WA KANDO
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769

                                                                          SEHEMU YA PILI

Ipoishia.......macho yao yakakuta mwili wa mwanaume ukiwa chuni..
Songa nayo.........
Mwili huo ulikuwa umechomwa visu mara tatu kifuani na tumboni ,mbali na hivyo ,maiti yake ilibuluzwa na kuacha michirizi ya damu pale chini .Kila mmoja hakuamini alichokuwa anakiona ,ilikuwaje mwanaume huyo auwawe ndani ya nyumba ile halafu muuwaji asionekane?Kitu cha kwanza kabisa ,hawakugusa mwili ule wakatoka ndani na kuelekea katika kompyuta zao na kuangalia orodha ya watu walioingia ndani ya hoteli hiyo dakika chache zilipita kwani maiti ilivyoonekana ,haikuonekana kama iliuwawa muda mrefu uliopita "
"Mmeangalia jina lake?"
"Hapana"
"Hebu kampekueni mnaweza kuona hata kitambulisho '"alisema  mwanaume aliye shika kompyuta mpakato na hivyo walinzi hao kurudi ndani ya nyumba hiyo huku watu wengine wakiwa nje na idadi kubwa ya watu ikizidi kuongezeka
Walipoingia humo ,wakampekua mfukoni na  kukuta "business card"iliyomtambulisha kwa jina la OMARY HEMED ,mwanaume wa kiarabu aliyekuwa akimiliki kampuni kadhaaa ikiwemo ya cotton
"Kumbe ni Omary !"alisema mwanaume mmoja kwa mshangao.
"Ndiye nani?"
"Yule bilionea wa kiarabu!"
"Unamaanisha yule mwenye utajiri wa bilioni kumi na mbili ?"aliuliza mlinzi mwingine
"Ndiyo!"
"Mh!hebu nione hiyo kadi
Akachukua na kuanza kuikagua kama alicho kiona mwenzake na yeye alikiona hivyohivyo .Kila mmoja alishangaaa ,hawakuamini kile walichokuwa wakikiona walifahamu sana matajiri .kila kona walipokuwa wakienda walienda na walinzi wao ilikuwaje OMARY aende huko peke yake mpaka kuuwawa?kila walipojiuliza wakakosa majibu wakatoka nje wakiwa na ile jadi na walipomuonyesha jamaa aliyekuwa na kompyuta akaangalia jina lile akagundua jina lile OMARY alikuwa amekuja ndani ya hoteli hiyo na msichana mrembo aliyeitwa kwa jina la MARIAM aliyekuwa na asili ya Nigeria
"Aliingia na mwanamke humu ndani"
alisema jamaa huyo
'Hebu tuone "
Akaangalia kwenye kompyuta ile kwa lengo la kujiridhisha kile alichoambiwa  ndicho alichokiona .
Hawakujua mwanamke huyo alikuwa wapi kwani walikuwa na uhakika kwamba yeye ndiye aliyemuua OMARY na kisha kukimbia.
Wakawasiliana na polisi ambapo baada ya dakika kadhaa wakafika na kuingia ndani ya hoteli ile wakaelekea mpaka kule kulipokuwa na maiti ile kisha kuiangalia .Iliuonesha kwamba hakuuwawa mda mwingi uliopita na hata muuaji alikimbia
Wakapiga picha mwili ule kisha kuubeba kwa lengo la kuondoka nao ila kabla hawajaondoka wakaona kipande cha karatasi..........JE NINI KARATASI HIYO INA UJUMBE GANI USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA..

No comments:

Post a Comment