KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
SEHEMU YA KUMI NA TANO
JASHO lilikuwa linamtoka kwa fujo, kipande cha mgongoni kilikuwa kimelowana tayari na sasa tembe za jasho zilikuwa zinazidi kutumbuka katika uso wake. Mkono wake wa kulia bado ulikuwa unatetemeka na alihisi maumivu kwa mbali.
“Kile ni kichwa ama chuma?.” Nyelembe alijiuliza huku akijaribu kuurusharusha mkono wake katika namna ya kupambana na maumivu yale.
Haikusaidia, mkono bado ulikuwa unauma.
Wakati hili halijapita, adui yule ambaye alionekana kuzidiwa nguvu aliinuka tena, nab ado alionyesha wazi wazi kuwa ana ari ya kupambana.
Bwege ana roho ya paka shume! Nyelembe alijisemea huku akikiri kuwa sasa alikuwa anamuogopa.

“Kama huyu siye ninayemtafuta, huyo ninayemtafuta atakuwaje?” Swali likapeea katika fikra zake.
Jibu halikupatikana kabla hajavamiwa na yule bwana ‘tolu’ aliyemaanisha kuua ama kudhuru vibaya mno.
Nyelembe akajaribu kumkwepa lakini akawa mzito, ngumi moja ikamkung’uta kwenye bega lake, mkono tofauti na ule uliokuwa ukimchonyota.

Sasa maumivu yakawa katika mikono yake yote miwili.
“Kumbe rangi ya kifo nd’o mbaya hivi?” Nyelembe au Chuma chakavu alivyopenda kujiita akasema kwa sauti ya chini huku akiwahi kujiweka imara kukabiliana.
Akajaribu kuikunja ngumi yake walau kutoka katika mkono mmoja lakini akaishia kuzama katika maumivu makali sana.
Akasalimu amri akaacha kuendelea kufanya jaribio lile.
Tolu akamjia tena kwa kasi huku akiendelea kuzungumza kabila asiyowahi kuisikia nchini Tanzania. Jitu lile refu lilijikunjua huku likipiga kelele, meno yake meusi, yaliyo katika mpangilio wa hovyohovyo na mengine yakiwa yamepungua yalionekana.
Lilikuwa linaunguruma mithiri ya Mbwa aliyechokozwa na anajijua kuwa mapambano anayaweza. Likajitupa kwa nguvu zote kukabiliana na Nyelembe.
Nyelembe akaliona lilivyokosea ‘stepu’, akatabasamu na kuuona ushindi ukijileta kirahisi. Nyelembe akajizungusha ili aweze kutokwa na lile teke maarufu la kuzungusha mkuu kisha unyayo unatua katika kifua cha adui na kusababisha madhara makubwa.
Nyelembe akajirusha kwa akili zote timamu, lakini alisahau kuwa mwili wake haukuwa timamu tena.
Akaisikia suruali yake ikipasuka katikati, kisha akatua chini kama mzigo wa mchele wa plastiki uliolowana.
Nyelembe umezeeka aisee! Alijisemea huku akiona uchungu kuitoa kauli ile. Teke lile lilikuwa sawa sawia wakati wa ujana wake sio katika umri huo.
Nyelembe akajiona yeye kama yeye sio silaha tena inayotamaniwa na kila mpambanaji, akajiona si tena bunduki aina ya AK-47 inayopendwa zaidi na wapambanaji hasahasa vijana, akajiona yeye ni aina ya gobole lenye risasi moja, lisilosafishwa mara kwa mara, na sasa anataka kukabiliana na majambazi yenye nguvu mpya.
Kushoto kwake akauona msaada.
Jiwe!
Nyelembe akainuka upesi kabla lile jitu refu halijarejea kumshambulia, akatua katika lile jiwe na safari hii ilikuwa iwe ama la isiwe kabisa.
Bila kujali maumivu ya mkono wake akarusha jiwe lile kubwa kiasi likamfiki barabara katika uso wake, akatua chini akigaagaa.
Huo sasa ukawa wakati wa Nyelembe kugeuka kuwa kijana tena. mpenda masihara.
Mwenye majigambo mengi nyingi.
Zaidi aliamua kumkera.
Akamfikia kwa kasi na kumkalia nyuma ya mgongo wake, akakishika kichwa chake chenye jeraha na kuanza kukibamiza chini kwa kurudia rudia.
“Yakitoka meno manne naomba unikumbushe, mi kwa huku nyuma sioni vizuri” Nyelembe.... alimweleza yule bwana kwa utulivu kabisa.......JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA HAPA HAPA

No comments:
Post a Comment