- HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Wednesday, 18 April 2018



KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769


                                                   SEHEMU YA KUMI NA SITA...


Jamaa akabaki kuugulia maumivu na asiweze kujitetea. Nyelembe  akaendelea kumbamiza mpaka aliporidhika ndipo alipomgeuza.
“Kwa uzoefu wangu ni kwamba umeishi Tanzania kwa miaka mingi tu, haiwezkani walau maneno mawili matatu ya Kiswahili usiyajue, waha na wamanyema sio wabinafsi kiasi hicho eti useme muda wote wanaongea kabila zao, mbona wanaongea Kiswahili mara nyingi. Sasa tunazungumza Kiswahili ama la naku…..” Akaiacha ile kauli ikielea na mara akakiruhusu kichwa chake kikamtandika yule bwana ipasavyo.
Jino likatoka!
“Hili jino la ngapi limetoka, naona kama nachanganya mahesabu yangu.”
“Nisamehe… samehe sijui kitu” jitu refu likatokwa na maneno yale kwa shida.
NYELEMBE akacheka kwa tuo, kisha akalitazama usoni.
“Naitwa Nyelembe wengi wanapenda kuniita chuma chakavu najua unajua maana ya chuma chakavu hakithaminiwi kabisaa, ni baba wa mtoto mmoja. Mke wangu ananiita baba watoto licha ya kwamba nina mtoto mmoja tu. Najua huwa ananidanganya bila kujua. Ni mke wangu pekee anayenidanganya na ninaridhika. Wewe ukinidanganya kwa kujua ama kutojua nitakuua katika namna ambayo haujawahi kuuliwa hapo kabla…..” akatulia kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea.
“Nijibu kwa uzuri kabisa hadi sasa mmeua watu wangapi?”
“Sijui Swahili muzuri kaka yangu, samehe mimi ni binaadam” Akajibu kitu ambacho hajaulizwa.
Pole za dhati zimfikie popote alipo, kwani hakumjua vyema aliyekuwa mbele yake..Asalaleee nafikili wengi mnajua pale simba mwenye njaa kali napomkamata swala au mnyama yoyote ambaye atapita katika mawindo yake..sasa ndo kilicho mkuta bwana huyu ambaye alionesha kuwa hakuwa anakielewa kiswahili vizuri hiyo haikuwa tatizo la kwamba yeye akwepe kifo ambacho kilikuwa mbele yake wakati wao wamefanya mauaji kwa watu ambao hata kujitetea hawawezi ..Nakuuliza mala ya mwisho mlikuwa mnawapa nafasi ya kujitetea wakati mlipokuwa mnataka kuwauwa ...'Mkuku mimi jui kabisa samehe mimi"Wakati anamaliza kuzungumza alikuwa tayaria anawasalimia walio tangulia mbele za haki "aaaah watu wengine bhana huwa wanashindwa tu kusema mpaka wapate mateso kama haya jamani "Aliongea huku akiwa anatabasamu kana kwamba kitu alichokuwa ametoka kukifanya kilikuwa ni cha kufurahisha...huyo ndo alikuwa Nyelembe ambaye ameamua kuingilia kati kulisaidia jeshi la polisi kufanya kazi ....USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA ILI KUJA HATIMA YA MKASA HUUU

No comments:

Post a Comment