- HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Monday, 16 April 2018

KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769

                                                           SEHEMU YA KUMI

Mala baada ya gari ile iliyokuja kuchukua mwili wa mke wangu na kutoweka kwa kasi ya ajabu ndipo na polisi walikuwa wanafika mda huo baada ya tukio na kuaanza kumuhoji huku wakikagua nyumba yake kwa kuanza kuhisi kuwa huenda kwa namna moja huyu na yeye atakuwa anahusika na mauaji yale ambayo yanaendelea nchi nzima....
Mwenyekiti wa mtaa aliokuwa akiishi Yusuph ambaye amepotelewa na familia yake aliye julikana kwa jina la chuma chakavu sikujua kuwa jina hili lilikuwa likimaanisha kitu gani au lilikuwa linamaana gani maana pia alishuhudia tukio zima pamoja na Yusuph anaguswa na kile alichokiona wakati Yusuph  akifanyiwa ukaguzi katika nyumba yake......na maaskari ambao walikuwa wameshachanganyikiwa.....
Anaamua na yeye kuingilia kati mkasa ule ili kumsaidia Yusuph ambaye kwa sasa alikuwa matatani bila kujari hatari yoyote

NI kwa wale waliokuwa wakiishi dunia ya peke yao nd'o wasingekuwa na la kuongea juu ya sekeseke lililomkumba mkuu wa mkoa wa Tabora sekeseke ambalo lilisababisha bwana yule kuwa kama mwendawazimu anayezurura kuhu na kule..
Lakini pia kwa wengine ikiwa faida kwao kuweza kumuona mkuu wao wa mkoa kwa mara ya kwanza. Ilikuwa si rahisi kumwona bwana huyu ambaye aliishi kifalme na kuacha maswali kwa wananchi juu ya kitu gani ambacho aliyemteua alikiona hadi akamtupa katika cheo hicho kikubwa???
Sasa alikuwa anaonekana bila hiari yake!
Watoto wake wawili ambao ni mapacha  walikuwa wametoweka ghafla na wasijulikane ni wapi walikuwa.
Msaada wa kwanza ulikuwa kuliamuru jeshi la polisi kufanya msako yakinifu!
Holaa! hakuna walichoambulia.
Kushindwa kwa jaribio hili kukawafanya watafute njia mbadala ya kujisafisha waonekane wanatenda kazi ipasavyo, wakaanza kufanya kamatakamata ya yeyote ambaye waliamua kumtilia mashaka.
Rungu hili likawaangukia vijana wakaa vijiweni na wale wazururaji.
Raia walilalamika, haikuwa mara ya kwanza tukio la namna hii kutokea. Hapa zikaanza kuzuka tetesi kuwa kuna makablasha kadhaa yamefunguliwa polisi juu ya watu kupotea lakini yamelazwa huko yakinyonya vumbi huku jibu jepesi likiwa uepelelezi unaendelea.
Jalada mojawapo likiwa ni lile lililofunguliwa na Yusuph ambaye sasa anahesabika kama mshukiwa wa tuhuma hizi
Ama kwa hakika dunia haina usawa!
Kilio cha Yusuph hakikuweza kuwa msaada kwake, alizidi kuonekana kuwa anahusiana kwa namna moja ama nyingine na yule muuaji ambaye hajulikani anaua kwa nini na bahati mbaya zaidi hakuna ajuaye kama kweli anaua ama anaiba watu....
Yalibaki majibu yaliyozaa maswali.
Waliojiuliza nd'o haohao walitakiwa kujichagulia majibu.
Mwisho kila mmoja akamrejea Mungu wake na kuombea yale madhira yasije yakamkumba yeye ama yeyote katika familia yake.....
SAKATA la watoto mapacha lilikolea baada ya viatu vya watoto wale kukutwa jirani na nyumba ya kulala wageni iliyokuwa jirani na mji wa Urambo mkoani Tabor
.
Pole kwa wote waliolala katika nyumba hii siku hiyo, hii ikawa ni siku ya waliozoea kujificha katika nyumba zile na kufanya maasi na wake za watu na waume za watu kujulikana.
Polisi waliizingira ile nyumba, wakaanza na muhudumu wa pale mapokezi na kisha ukafuata msako wa chumba kwa chumba.JE NINI KITAENDELEA SIMULIZI YETU INAZIDI KUSHIKA KASI USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA

No comments:

Post a Comment