- HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Sunday, 8 April 2018

KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769


                                                                     SEHEMU YA PILI

Kutokana na dada yule kuwa uchi wa mnyama halafu na sehemu ile ilikuwa na baridi sana nikaona nimpe koti langu ambalo kwa namna nmoja ama nyingine lingeeza kumstili .kwani ilikuwa imetimu majira ya saa sita usiku huku tayari nikiwa nimeshaanza kumkumbuka mke wangu nyumbani ambaye nimkorofi sana na ni mwanamke mwenye wivu mkali ..Nikamchukulia chumba dada yule kwa lengo la kuwa kesho niongee nae ili anieleze mkasa wake kisha nikampatia na kiasi kidogo cha pesa cha kutumi akipata dharura kisha nikaondoka zangu na kuelekea nyumbani kwangu..Niligonga zaidi ya mala tatu nilipoona mke wangu afungui mlango nikaamua kujaribu kumpigia simu iliita kwa mda kisha ikapokelewa na sauti ambayo ilionekana wazi kuwa ilikuwa imetoka usingizini..
Mke wangu ni mimi Omary niko nje nimegonga hadi nimechoka nakuomba uje unifungulie"
nilimaliza kisha nikakata simu "Baada ya mda kidogo mke wangu alikuja kufungua huku akionekana kuwa ni mwenye uchuvu mwingi sana'baada ya kufungua mlango yeye alitangulia kuingia ndani na kuniacha mimi nikimfuata kwa nyuma .Mbona hauna koti leolilikuwa ni swali la kwanza kabla ya salamu kutoka kwa mke wangu.
Nilijikuta nikikosa jibu la kumjibu kwani niseme kuwa nilimsaidia mwanamke aliyekuwa uchi hapana hii itazua utata'
Nikajalibu kutumia uongo wangu wote kuwa nilikuwa nimelisahau ofisini hii ni kazi ambayo niliipata baada ya kuacha kazi ya uaskari jeshi..Mke wangu alinielewa lakini kwa shingo upande.Majira ya asubuhi kwani mimi hupenda zaidi kufanya mazoezi ya mwili kila siku niamkapo lakini siku hii ilikuwa tofauti sana kwani nilikuwa nimezoea kumkuta mke wangu akiwa tayari ameshaandaa chai hivyo mimi hufika na kupata kifungua kinywa hicho lakini siku hii nilimkuta mke wangu akiwa amekaa kwenye makochi huku akiwa kanuna kupita maelezo .Nikajifanya sijamuona na kutaka kupita ilikuelekea chumbani lakini akaniita John nikamgeukia na kumuuliza kulikoni akaniambia kuwa kuna hawala yangu kapiga simu alikuwa akiniitaji iliaweze kunishukuru kwa msaada ambao nimempatia jana usiku"mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakipiga kwa kasi aya ajabu huku nikijutia udnganyifu nilioufanya usiku wa kutomueleza mke wangu ukweli kuhusu tukio ambalo lilinikumba jana hadi kupelekea kutorudi na koti nyumbani sasa mke wangu alikuwa anielewi kabisaa nilijaribu kumueleza kuwa mimi sina mwanamke mwingine zaidi yake na ninampenda kwa dhati kwani nisingeweza kumsaliti.Lakini ilikuwa ni sawa na kuchochea moto mke wangu sasa aliwaka na kuwa kama mbogo huku akidai kuwa nimpeleke hadi kwenye hiyo nyumba ya kulala  wageni ili yeye mwenyewe akajionee kama ninayoyasema niyakweli au namdangaya ....KIZAZAA KIMEZUKA KATIKA FAMILIA YA JOHN JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA

No comments:

Post a Comment