KOSA LANGU
MWANDISHI :ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ni majira ya jioni nikiwa nimekaa katika moja ya bar ambazo ziko jirani karibu kabisa na nyumba yangu hapo tayari nilkuwa nimegida chupa zipatazo nne za bia na hapo nilikuwa nikikisikia kichwa changu kikiwa kimechangamka angalau niliweza kuhisi kuwa mzigo wa mawazo ukiwa umepunguwa .Hiyo ilikuwa kama nikanuni ambayo nilikuwa nimejiwekea kila siku kama nitakuwa nimetigwa na mawazo nilazima angalau nipate moja baridi moja moto .Nikiwa namalizia chupa yangu ya nne alifika dada mmoja na kuomba kama sitajali aweze kujumuika nami katika meza ile nilimjibu huku nikiwa bado nimeinama kwani sikuweza hata kutazama sula yake.Nikaitazma chupa yangu maana nilikuwa nakalibia kumaliza hivyo sikuona ajabu kumkaribisha "habari kaka"salama nilijibu huku nikipatanafasi ya kutazama usoni.Uso wake ulikuwa umejaa simanzi alisikitisha kiukweli lakini mimi sikujali.Baada ya kumkaribisha dada yule mda wote alikuwa ameinamia meza huku akiwa na chupa ya bia mkoni baada ya kama dakika kumi nilikuwa tayari nimeishainuka na kwenda kulipia gharama ambazo nilikuwa nimetumia
Dada bei gani?
Elfu nane mia tano tuuu
Aliongea kana kwamba ni hela ndogo basi nikampa noti ya shilingi elfu kumi?
Alianza kujizungusha akizani kuwa labda nitaiacha chenji iliyobaki lakini haikuwa hivyo
"Samahani dada unaweza kunpatia hiyo hela maana nachelewa"
"Sawa "alijibu kwa unyonge mhudumu yule kwani mimi sikuwa na kawaida ya kuacha hela yangu kwenye baa zote ambazo huwa napenda kwenda kuchangamsha akili yangu"Nikiwa njiani natembea mala nilisikia mtu akiwa analia huku akijongoe upande wangu hofu iliniingia kwani hakuwa mtu mmoja bali nilisikia vishindo vya watu kama watano"nikawa nimesimama pale pale bila kupiga hatua yoyote huku nikisubiri kinachoenda kujiri kwa wakati huo kwa mbali niliweza kumuona dada mmoja akiwa anakuja upande wangu huku akiwa uchi wa mnyama na nyuma yake niliweza kuona vijana wasiozidi watano wakimfauata na kumuomba asimame
"Tafadhari kaka yangu naomba unisaidie wanataka kuniuwa hawa"
"Hapana huyu ni ndugu yetu na tunataka kumrudisha shumbani maana amerukwa na akili"
"Hapana usiwasikilize hawa kaka yangu ni waongo wataniua nisaidie nakuomba kaka yangu"aliendelea kusihi dada yule ambaye haikuwa mala ya kwanza kukutana naye ila sikuweza kukumbuka niwapi nimemuona kutakana na pombe kuanza kuchukua nafasi yake katiaka kichwa changu nikiwa bado najiuluza nimemuona wapi dada huyu mala gafla nilishtukia nikiwa napigwa teke ambalo lilinopeleka hadi chini kisha nikajitahidi kuinuka kilevilevi"Broo tumekiumbia utuachie dada yetu vinginevyo utakuwa matatani"uliongea jamaa mmoja ambaye kidogo alionekana kuwa na mwili mkubwa kuliko wenzake
"Huyu dada amuondoki nae"nilijibu kwa kujiamini kwani kabla ya kuwa hapo tayari nilikuwa nimeshapitia mafunzo ya jkt hadi naacha kazi ya nilikuwa ni mwanajeshi hvyo bado nilikuwa na kumbukumbu za kukabiliana na maadui japo ni siku nyingi zimepita "
"Unataka kujifanya mjuaji sio "alizungumza kwa mala ya pili jamaa yule ambaye kwa sasa alionekana kuwa na hasira zaidi ya mwanzo ..Wakati tunaendelea kujibizana na yule bwana mmoja kati yao alikuja mbio kutaka kunilukia teke lakini nikalikwepa na kujikuta akianguka na kuugulia maumivu huku wengine pia wawili nikiwapiga ngumi ambazo niliziona kulingana na muonekano wao lazima ziliwatosha kabisaa kuwapeleka chini"nikatoa moja ya kitambulisho cha udereva nakukionesha kama askari wanavyo fanya wakiwa wanataka kumkamata adui basi kutokana na sehemu tuliyokuwepo ilikuwa inagiza kiasi ilitosha kabisa kuwaaminisha kuwa mimi ni askari na kuwafanya jamaaa hao kukimbia na kuniacha nikiwa nimechoka
"Asante sana kaka yangu umeniokoa "Alikuwa akiongea dada yule
"Usiku huu unaelekea wapi"!nilihoji
"Naelekea mkoani mbeya kwani ndiko ndugu zangu waliko"
Umetoka wapi usiku huu!
Kaka yangu nistori ndefu sana ............USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Sunday, 8 April 2018
New
About Hamadi abel
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment