MAMA NI MAMA
MWANDISHI: ISSA JUMA
WHATSAPP NO:0743924769
Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa na chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa na chongo .Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania .Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.Lakini mama alimpenda mwanae alipomnyanyapaa waziwazi .Baadae mtoto akakuwa akamaliza masomo yake na kupata kazi nzuri akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake chongo anayemtia aibu .Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake.Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa `mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa katika jamii yake .Siku moja asubuhi wanae wakilia walipokua nje wakicheza.Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha .Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae .Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja .Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi .Alipomtizama akagundua kuwa ni mama yake mzazi.Alikuwa amechoka na amezeeka sana amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa mtoto kwa hasira akamuuliza"mama umekuja kufanya nini hapa"kama una shida ungenipigia simu sio kuja ?kwanza nani kakuonehsa napo ishi ?Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango?Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako"mama yake akasema"samahani mwanangu sikujua"Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.Baada ya siku chache kupita yule jamaa akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona .Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akamsikilize mama yake anasema nini .Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao .Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua bila msaada wowote.Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake barua ilisomeka hivi.....Kwa mwanangu mpendwa wa pekee ,Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui kama nitapona nimeugua nikakosa matibabu kwa kukosa pesa sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida zangu zaid yako wewe lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie ulinifukuza na kudai nawashitua wanao kwa chongo langu.Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana....nami sikubahatika kupata mtoto mwingine nilikulea kwa nguvu zangu zote nikitegemea baadae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ,hivyo unaona aibu kuwa nami...nisamehe kwa kuwatisha wanao nisamehe kwa kuja kwako bila taarifa ,nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio ,lakini naombo nikupe siri ambayo ulikuwa huifahamu .Mwanangu wewe ndiye uliyezaliwa chongo ulikuwa na jicho moja tu .nikaona ni kheri mimi niwe na jicho moja ili wewe uwe nayo yote mawili.Naulipowekewa jicho langu nilifurahi kukuona una macho mawili nikajua utaweza vema kuziba changamoto za dunia hii,na hakika jicho langu limekusaidia wewe ni mtu mashuhuri na tajiri sana kwa sasa lakini kwa jinsi ninavyoumwa nitakufa .Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu .Wasalimie wajukuu wangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu .Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana .Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema alio mtendea lakini haikuwezekana ........KWA MAONI USISITE
Sunday, 18 March 2018
New
MAMA NI MAMA
About Hamadi abel
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment