UNIVERSITY LIFE - HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Saturday, 17 March 2018

UNIVERSITY LIFE

UNIVERSITY LIFE
MWANDISHI:ISSA JUMA
WHATSAPP NO:0743924769

                                                     SEHEMU YA KWANZA(1)
Baada ya kuwa nimehitimu elimu yangu ya kidato cha sita nilichaguliwa kwenda kujiunga na chuo kikuu cha dodoma(udom).Nilikuwa natokea katika familia ya kawaida sana ambayo ilikuwa inajihusisha hasa na shughuli za kilimo mkoani Singida.
Baada ya mwezi mmoja nilikuwa tayari nimeripoti chuoni mazingira yalikuwa mageni sana kwangu kwani ilikuwa mala ya kwanza kufika mkoani dodoma .Nilifika katika ofisi za chuo hiko na niliweza kupangiwa sehemu ambayo nitakuwa nikiishi siku zote ambazo nitakuwa chuoni hapo nilipangiwa chumba kimoja na wanafunzi wenzangu wanne katika chumba kile.Nilikaribishwa na wale wanafunzi niliyo wakuta katika chumba kile wakaanza kujitambulisha
Mwanafunzi wa kwanza:Oyaaa mi naitwa Juma niko mwaka wa kwanza na chukua uhasibu apa.Alimaliza kujitambulisha.

Mwanafunzi wa pili:Huyu alianza na salamu baada ya hapo alijitambulisha mimi naitwa Mkumbo karibu sana mimi nachukua ualimu wa shule ya msingi apa.Huyu alionekana kuwa ni mtu wa dini sana.

Mwanafunzi wa tatu:Asee chalii karibu sana mi natoka Arusha aseee nachukua ualimu kama huyo mchungaji karibu sana chalii.Alimaliza kwa utambulisho wake ilifika zamu yangu kujitambulisha kama wenzangu walivyo fanya chumba chote tulikuwa mwaka mmoja hivyo sikuwa na wasiwasi sana na wale wenzangu niliyo wakuta mle katika kile chumba.
Mimi naitwa Abeli natokea Singida niko hapa nasomea uhasibu.Mala Juma akadakia asee mimi ndo nitakuwa mwalimu wako hapa mpaka utakuwa mjanja kama mimi au unasemaje Abeli jisikie uko nyumbani. Juma aliendelea kuzungumza uku akioneka kama ndo uzungumzaji sana katika kile chumba uku mimi nikiendelea kupanga nguo zangu katika kabati langu na Mkumbo akiendelea kusoma kitabu kitakatifu kama nilivyo sema mwanzo huyu alionekana kuwa mtu wa mungu sana.

Baada ya wiki moja nikiwa nimeshaanza kuzoea  maisha  ya pale chuoni kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wenzangu niliyo wakuta chuoni pale.Baada ya kutoka kipindi cha asubuhi nilikuwa naongozana na Juma maana wote tulikuwa tukisoma darasa moja tofauti na wale wengine ambao walikuwa wakisomea ualimu wa shule ya msingi.Baada ya kuwa tumepata chakula cha mchana mimi pamoja na juma tulikuwa njiani tukielekea bwenini mala tukakuta na msichana ambaye kwa mtazamo alionekana kuwa ni binti mzuri aliye kamilika kwa kila kitu si macho, pia alikuwa na umbo la kuvutia kila mwanaume atakaye mtazama.Kwa kuwa mimi bado nilikuwa sijazoea vizuri mazingira ya pale chuoni hivyo mwenyeji wangu Juma alianza kusalimia dada yule ambaye alioneka kutokujali salamu ya juma na kuendelea na shunguli zake.Daah uyu dada anajiskia sana ataki ata kuitikia salamu daah kweli watoto wa kishua wanatuchukulia sisi kama mbwaa jamaa angu ila hamna shida jamaa angu .
Baada ya kuwa tumefika katika chumba chetu tuliwaeleza wenzetu yaliyo tukuta tulipo jaribu kumsalimia dada yule walicheka sana hasa Mkumbo a.k.a baba paroko alicheka hadi akaanguka chini na kuanza kusema muwe mnauliza kabla ya kupalamia watu kwanza yule dada anasoma mwaka wa kwanza  alafu anasomea sheria chuoni ,pia ni waziri mkuu chuoni hapa alafu ni mtoto wa makamu wa rais wa Tanzania hivyo lazima ajisikie ...hahahahahahahahahahahahahahahah tulicheka kwa pamoja kwa kitendo cha kuonekana mbwa mbele ya binti yule aliyekuwa akitokea katika familia ya kitajiri.Hivi kwanza anaitwa nani mimi(Abeli)niliuliza Mkumbo akajibu anaitwa Yasinta duuuh niliguna na kusema anajina zuri sanaa wakati wote tunajadili kuhusu dada yule Sospeter a.k.a chuga boy alikuwa kimya sana akituangalia na kutabasamu kisha akasema ndugu zangu yule mtoto ni lazima mimi niwe nae ata akiwa mtoto wa makamu sijui waziri mimi sijali

Wote wakashangazwa na kauli aliyo toka nayo Chuga boy ................JE NINI KITAENDELEA
MAONI YAKO KUHUSU SIMILIZI HII NZURI YA KUELIMISHA NA KUSISIMUA ...










No comments:

Post a Comment