KOSA LANGU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
SEHEMU YA NANE
Iliopishia John na Omary ndani ya mkakati wa kuusaka uhuru wao kwa kumtafuta muusika wa mauaji yanayoendelea nchini.Songa nayo.......
Lilikuwa ni tukio la kushangaza sana kwani kila mtu alikuwa akisema kwajinsi alivyokuwa akijua yeye mwenyewe wengine walisema kuwa amewatoa kafara watoto wake ili ashinde katika uchaguzi mkuu ..na wengine walisema kuwa hawakuwa watoto wake ..Lilikuwa ni tukio la kupotea kwa watoto wa mkuu wa mkoa wa Tabora ambaye ilisemekana kuwa alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu. Kwani ilisemekana kuwa watoto wale walitoweka katika mazingira yaliyo tatanisha na hivyo hakuna mtu aliyeshuhudia tukio hilo la kupotea kwa watoto wale wawili ...
Jijini Dar es salaam ,,,tulikuwa katika moja ya nyumba ya kigogo mmoja aliye kuwa akionekan kuwa na uhusiano wa karibu sana na chama tawala .wakati wote tuliokuwa tumesimama pale mimi nilikuwa sijaelewa nini lilikuwa kusudio la Omary kwani mda wote hakusema chochote zaid ya kuniambia niwe makini katika kumfuatilia yule bwana ambaye alionekana kuwa mwenye asili ya kiarabu pia alikuwa na walinzi wasio pungua wanne ,gari yake lilikuwa jeusi na lenye tintedi nyeusi hivyo ilikuwa ngumu kugundua aliyekuwa ndani ya gari hilo mpaka pale aliposhuka bwana yule mwenye majigambo sana tulikaaa kwa mda wa masaaa zaidi ya mawili pale lakini cha kushangaza bwana yule hakuoneka kutoka ,mpaka mimi nilipoanza kulala mika kuwa nahisi njaa halafu nimechoka kukaa sehemu ambayo haikuwa ikitupa mwanga wa lile ambalo tulikuwa tukilifuatialia
Lakini Omary alisihi kuwa tuendelee kuwa wavumilivu kwani ule ulikuwa ni mwanga wa safari yetu ..
Mkoani Tabora bado askari walikuwa katika msako wa kuwatafuta watoto wa mkuu wa mkoa huyo bila kukata tamaa japo dalili ilionesha kuwa hakuna uwezekano wa kuwapata watoto wale lakini askari wale hawakukata tamaaa kwa sababu ilikuwa ni amri kutoka kwa mkuu.Linazuka tukio jingine la kupotea kwa basi la abiria ambalo huwa linafanya safari zake kutoka Kigoma hadi Tabora kila siku lakini zinafika taarifa za kupotea kwa abiria waliokuwa ndani ya basi lile bila kuwa uhakika zaidi kuwa walikuwa wametekwa na majambazi au wamepotea katiaka mazingira gani..Taarifa hizo zilizidi kulipa wakati mgumu jeshi la polisi pamoja na kutupa sisi pia kazi ngumu ya wapi tunatakiwa kuanzia ilikufanya kazi yetu kwa sababu leo unasikia mkoa huu kesho mkoa mwingine ilikuwa ni pasua kichwa kwa kweli nahisi aliyekuwa akifanya haya alikuwa anaijua vizuri serikali hivyo alifanya ilikuikomoa kabisa ..
Tunarudi mkoani kigoama ..Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwani nilikuwa nimekaa na familia yangu katika ki baraza cha nyumba yangu tulikuwa tukipata chakula cha jioni mimi pamoja na mke na mtoto mmoja ambaye nilikuwa nikimpenda sana ..baada ya kuwa tumemaliza kupata chakula mke wangu aliomba kwenda chooni ..nikataka kumsindikiza lakini akasema kuwa anaweza kwenda mwenyewe huku akiwa ni mwenye furaha sana ..kelele za kuomba msaada zilisikika na ilikuwa ni sauti ya mke wangu ambayo ilikuwa ikiomba msaada....USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA HAHA KATIKA KUNDI LANGU LA SIMULIZI
Friday, 13 April 2018
New
About Hamadi abel
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment