CHOMBEZO:JAMANI MWALIMU
MWANDISHI:ISSA JUMA
WATSAPP NO:0743924769
SEHEMU YA TANO
Ilipoishia Yasini anakutana na Yasinta wakati akiwa katika matembezi yake *******
Inapoendelea .....Yasinta aliipita katika duka la mangi kuweza kununua alichokuwa akitaka kununua ikabidi na mimi nipite japo sikuwa na lengo la kufanyamatumizi ya aina yoyote ilinibidi nichukue pipi aina ya big bom(pipi ya mti)yeye Yasinta alikuwa akinunua akinunua soda pamoja na keki mala baada ya mda Yasinta alikuwa akijipapasa mifukoni mwake akiwa kama mtu anae tafuta kitu fulani ambacho kili kuwa hakionekani yaani alikuwa amekosa hela ya kulipia vile vitu alivyo kuwa amenunua .....Nikaona hii ndo chansi ya kumpata mtoto huyo ikabidi nijipekuwe mfukoni na kutoa noti ya shilingi elfu tano nikamlipia vitu alivyokuwa amenunua na baada ya hapo tukawa tunazungumza huku tukiwa tunaelekea nyumbani kwao .....Hivi Yasinta lile jibu langu utanipa lini maana usiku mzima silali nakuwaza wewe ...mmmmh jamani Yasini umeanza habari zako ambazo mimi nilikuwa tayari nimeshakuambia kuwa nitakujibu siku ambayo mimi nitakuwa tayari kuwa na wewe ila asante kwa msaada ulionipa ..nafikiri tutaonana kesho shule...Yasinta akawa ameondoka na kuniacha nikiwa nimwzubaa nikikosa la kufanya....maana alivyokuwa ameumbika hapo ndipo palipokuwa pana niumiza zaidi yani mtoto mzuri kiasi hiki kunitesa kama mtoto mdogo...
Siku iliyo fuata shuleni kulikuwa na maonesho ya wanafunzi kuonesha vipaji walivyonavyo .Baada ya kama masaa mawili kuwa yamepita shughuli zikaanza wanafunzi mbalimbali walikuwa wakionyesha vipaji vyao huku wakishangiliwa wanao fanya vizuri na waliokuwa wakifanya vibaya walikuwa wakizomewa .Ukumbi ukakaa kimya huku tukiwa subiria washiriki wa shindano la umiss wa shule kupita mbele yetu huku majaji wakiwa ni waalimu wetu wa michezo pamoja na wanafunzi baadhi
Wakaanza kuingia mmoja mmoja huku wakiwa wamependeza ,nikajikuta ninanyanyuka kwa furaha huku nikipiga makofi hii ni baada ya kumuona Yasinta akiwa katika msururu huo wa mamisi wa shuleni hapo waliokuwa wamechanganyika vidato mbalimbali .
Wakajipanga mbele ya majaji na kuanza kuulizwa maswali mbalimbali.Ikafika zamu ya Yasinta wanafunzi wote walikaa kimya huku wakiwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi wao atakacho kijibu
Swali":Yasinta unaweza kutuambia upendo ni nini?
Yasinta:Upendo ni hali ya msukumo wa kihalisia kwa jinsi tunavyo hitaji.Hatuwezi kulazimisha ,kukomalia au kutawanya upendo kwa kadri tunavyoweza asante
Ukumbi mzima ulikuwa ukipiga makofi kasoro mimi nilijikuta nikiludia sentensi ya mwisho aliyosema "huwezi kumfanya mtu kukupenda"daah apa kanilenga kabisa mimi maana mimi ndo ninaye mkomalia kunipenda.Mda wa kutagazwa mshindi uliwadia na Yasinta kutangazwa kuwa mshindi daaah kwakweli Yasinta alikuwa amependeza kupita siku zote ambazo nilikuwa nikimuona .Mda wa kucheza ulifika hivyo Yasinta aliombwa kufungua ukimbi kwa kumchagua mtu wa kucheza nae ukumbi mzima ulikaa kimya kusuniri nani atakaye chaguliwa na mrembo huyu pia miss wa shule yetu mala Yasinta akanyoosha kidole kuelekea nilipo kuwa nimekaa nakunifanya nijisikie furaha sana kwa kupata bahati adimu kama ile nilipo taka kuinuka Yasinta akanyoosha kidole kushiria kuwa sikuwa mimi aliyekuwa akininyooshea kidole kumbe alikuwa akimnyooshea kaka mkuu wa shule kitendo ambacho kilinikela sana na kutamani dunia ipasuke niingie ...Jamaa akainuka kwa furaha sana maana alikuwa anataka kunikomoa mimi maana alijua ndo mtu ambaye nilikuwa karibu na Yasinta ..kabla kaka mkuu ajafika mbele kwa ajili ya kucheza kilitokea kitu ambacho hakuna aliye amini kama kingetokea ...JE NINI KIMETOKEA USIKOSE SEHEMU INAYO FUATA MAANA JAMANI MWALIMU IMEZIDI KUWA HATARI ZAIDI KADRI TUNAVYOSONGA ..
Friday, 23 March 2018
New
JAMANI MWALIMU
About Hamadi abel
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment