Taarifa ya Mamlaka ya Chakula Kuhusu Usalama wa Matumizi ya Maziwa ya Nido
TFDA imebaini uwepo wa taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kuogofya wananchi juu ya usalama wa maziwa ya Nido. Taarifa hiyo ina picha ya kopo la maziwa ya Nido na Inasema kuwa katika maziwa hayo kumewekwa vionge vya kulewesha.
Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa uchaguzi wa awali umeonyesha kuwa taarifa hii kwa sasa haina ukweli wowote.
TFDA kupitia mifumo yake ya ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa katika soko inaendelea kufuatilia bidhaa hii ikiwa ni pamoja na taarifa zinaazosambazwa.
Rai yetu kwa wananchi ni kuacha kusambaza taarifa zozote zinazohusu usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi bila kupata ufafanuzi na uthibitisho kutoka TFDA.
Imetolewa na;
Mkurgenzi Mkuu,
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),
Barabara ya Mandele- Mabibo External,
S.L.P 77150, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment