Mbowe afunguka na kusema kwa sasa Tundu lissu anaweza kunywa na kula - HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Thursday, 14 September 2017

Mbowe afunguka na kusema kwa sasa Tundu lissu anaweza kunywa na kula


Nairobi. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hivi sasa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaweza kuongea na kula kidogo.

Akizungumza na waandishi leo Alhamisi jijini Nairobi, Mbowe amesema taarifa za kwamba Lissu amepata maambukizi katika kifua ambayo yanatishia maisha yake siyo za ukweli.

Mbowe amesema hali ya Lissu inabadilika kila siku hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake.

Amesema Lissu ameweza kuonana na baadhi ya waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.

"Pamoja na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema Mbowe.

No comments:

Post a Comment