HIVI NDIVYO MWANAMKE ANAVYOWEZA KUBEBA MIMBA SIKU YA HEDHI.
Wengi najua mmeshangaa sana kuona hii post lakini huo ni ukweli mchungu unaofanya watu wanakana watoto na kuacha ndoa zao kwa kudhani wamesalitiwa wakati mimba ni zao na watoto ni wa kwao wenyewe.
Kwenye blog hii nimeshaongelea zaidi ya mara mbili mambo haya ya kuhesabu siku zako za hatari lakini hili sikulizungumzia, basi hebu twende sawa upate kunielewa vizuri na kama hukusoma hizo za nyuma na hujui kuhesabu siku zako za hatari soma hapa
Nilisema kwamba wanawake wote, siku yao ya hatari ya kubeba mimba ni siku ya 14 kabla ya kuona mzunguko unaofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita kama mnavyodanganyana mtaani.
Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla ya siku ya kumi na nne na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari, hivyo siku zingine za hatari ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.
Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama mzunguko wako ni mfupi, [ hapa ndio mtu anaeza anabeba mimba kwa kushiriki ngono akiwa kwenye hedhi], mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu. sasa kama mtu huyu anaona hedhi kwa siku nne afu akatembea na mwanaume siku ya nne au ya tatu wakati damu inaendelea kutoka basi mbegu za mwanaume zitaishi mpaka siku ya saba na kukutana na yai la kike ambalo litashuka siku hiyo ya saba na mimba kutunga, hivyo kama hufuatilii mzunguko wako akibeba mimba siku ya hedhi usishangae.
Mwisho: nimeandika hii makala makusudi kwani najua kuna watu wanatabia za kufanya ngono kipindi cha hedhi au wakati hedhi iko inaisha au tarehe za mwanzo baada ya hedhi kuisha wakidhani mimba haiwezekani basi leo taarifa ni kwamba inawezekana cha msingi fuatilia mzunguko wako vizuri usije ukaanza kusumbua watu ukishanasa mimba ambayo hukuipanga.
Comments
Nisaidieni me nahtaj mototo na nafanya cku us Hatari before and after lakini cpati ujauzito
ReplyDeleteNaitaji kuuliza je ikiwa umeingia siku ya 12na siku ya 16 nikakutanae je naweza kupat mimba
ReplyDeleteOk nimeelewa
ReplyDeleteMbona mnatuchanganya kwann mseme kabla ya kuona mzunguko ndio most mimba inaingia Mara wengne baada ya kuona hedh Siku 14 ndio mimba inaingia
ReplyDeleteMe mwenyewe hata sielewi
DeleteSamahan mm naomba kuuliza mwanammw anaweza kusex siku ya kumi na tatu kwa kutumia condom na akapata ujauzito Na ukiangalia mzunguko wake n wa sku 28??
ReplyDeleteMimi mzunguko wangu ni siku 24,nimefanya ngono siku ya tano,lkn siku ya 7 nimeona bleed zile zamwishoni tunaitaga sisi,,je kuna uwezekano wa mimba kuingia?
ReplyDeleteMe ata sielewi
ReplyDeleteDu na ukufanya mapenz siku ya mwwisho ya hedhi waweza pata mimba
ReplyDeleteKama ndoivyo.kwa mda ganii unaweza pata mimba baada ya dam ya abortion kukata
ReplyDeletembegu ya kiume ina uwezo wa kukaa siku 5, naomba kuelewa zaidi maana nilisoma kua ni masaa 72.. hii imekaje
ReplyDelete