Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Give Me’ ameiambia Bongo Dot Home ya Times Fm kuwa mashabiki wanaingilia kitu wasichokijua kiundani kitu ambacho si sawa.
“Ukweli ni kwamba hawapaswi kunizungumzia na yeye kwa sababu wakati tulikuwa tunatengenezana tulikuwa wawili, kwa hiyo huwezi kuingilia wewe kama shabiki maandazi kwa kuingilia vitu ambavyo huvijui.
“Mimi na yeye tulikuwa tunafahamiana wakati tupo chumbani, katika chumba cha studio lakini bada ya hapo tukawa wakubwa, sasa wewe shabiki ambaye unazungumza unamjua yeye? au unanijua mimi?, au mimi na yeye ndio tunajuana zaidi?,” amesema.
Ameongeza kuwa, “kwa hiyo wewe unaingia kati baada ya kumfahamu Bob Junior na huyo muhusika (Diamond), unaanza kumtetea yeye au kunitukana mimi wakati sisi hatuwafamu”.
Bob Junior amekuwa akimshutumu Diamond kwa kutangaza kuwa kuna kolabo ambayo wangefanya pamoja lakini hakuna utekelezaji na anapomtafuta ili kuzungumzia hilo amekuwa akimpuuza.
No comments:
Post a Comment