William ngeleja ajisalimisha baada ya kutajwa kwenye ripoti ya Tanzanite na almasi - HAMADI BLOG

Breaking

Random Posts

BANNER 728X90

Monday, 11 September 2017

William ngeleja ajisalimisha baada ya kutajwa kwenye ripoti ya Tanzanite na almasi


Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amehojiwa kwa saa moja katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 11.

Ngeleja ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu ya nne, aliwasili katika ofisi hiyo saa nne asubuhi akiwa peke yake ambapo alikutana na DCI saa tano na kuondoka saa sita na nusu mchana bila kusema alichohojiwa.

Hatua ya Ngeleja kufika ofisini hapo ni kuitikia wito wa Mkuu wa Jeshi La Polisi (IGP), Simon Sirro ambaye aliwataka watuhumiwa waliotajwa katika ripoti ya Tanzanite na Almasi kuripoti kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya mahojiano wakati uchunguzi ukiendelea

No comments:

Post a Comment